ASACOHUB
ASACOHUB
ASACHIFU COLLEGES HUB, Loading....
📞 +255 679 852 485  |  ✉ info@asacohub.ac.tz
About Contact Help
FAQ

Maswali Yanayoulizwa Sana

Hapa utapata majibu ya haraka kwa maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu ASACOHUB, wanafunzi, vyuo, malipo, na usalama.

27 Maswali 5 Makundi

Kwa Wanafunzi

Maswali 6 kwenye kundi hili

1 Je, kutumia ASACOHUB ni bure?
Ndiyo! Kwa wanafunzi, kujiunga na kuomba vyuo kwenye ASACOHUB ni bure kabisa. Huna kulipa kitu chochote ili kutumia jukwaa letu. Vyuo ndio hulipia lead ili kupata taarifa zako za mawasiliano.
2 Ninaweza kuomba vyuo vingapi?
Unaweza kuomba vyuo hadi vitatu (3) kwa wakati mmoja. Hii inakupa nafasi ya kuchagua vyuo vitatu unavyopenda. Ukishajibiwa na chuo kimoja, unaweza kuomba tena kama unataka.
3 Nini kinatokea baada ya kuomba?
Baada ya kuomba: (1) Chuo kinapokea maombi yako kama lead, (2) Chuo kinaona taarifa zako za kielimu (bila contacts), (3) Kama chuo kinakubali, kinalipia lead na kupata contacts zako, (4) Chuo kinawasiliana nawe, na (5) Unaweza kulipia application fee na kupata admission.
4 Kwa nini chuo hakiwezi kuona namba yangu ya simu kabla ya kulipia?
Tunalinda taarifa zako za mawasiliano. Chuo hakiwezi kuona namba yako ya simu, barua pepe, wala anwani yako hadi kilipie lead. Hii inazuia vyuo kukupigia ovyo ovyo bila wewe kutaka. Ni sehemu ya usalama wa taarifa zako.
5 Je, ninaweza kufuta akaunti yangu?
Ndiyo, unaweza kufuta akaunti yako wakati wowote. Nenda kwenye profile yako na uchague "Delete Account". Taarifa zako zote zitafutwa kabisa kwenye mfumo wetu. Hata hivyo, hatuwezi kurudisha taarifa zilizofutwa.
6 Nini kitatokea kama wasifu wangu utakataliwa?
Kama wasifu wako utakataliwa, utapata taarifa kwa SMS na Email. Utaona sababu ya kukataliwa kwenye profile yako. Unaweza kusahihisha taarifa na kuwasilisha tena kwa uhakiki. Hii inaweza kufanyika mara nyingi kadri inavyohitajika.

Hukupata Jibu Unalolitafuta?

Wasiliana nasi moja kwa moja na timu yetu itakusaidia haraka.

Uko Tayari Kuomba?

Fungua akaunti yako bure na anza kuomba vyuo hadi 3.