ASACOHUB
ASACOHUB
ASACHIFU COLLEGES HUB, Loading....
📞 +255 679 852 485  |  ✉ info@asacohub.ac.tz
About Contact Help
FAQ

Maswali Yanayoulizwa Sana

Hapa utapata majibu ya haraka kwa maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu ASACOHUB, wanafunzi, vyuo, malipo, na usalama.

27 Maswali 5 Makundi

Kwa Vyuo

Maswali 6 kwenye kundi hili

1 Ninawezaje kusajili chuo changu kwenye ASACOHUB?
Ili kusajili chuo: (1) Fungua akaunti ya chuo kwa jina la mwakilishi, (2) Jaza taarifa kamili za chuo (jina, NACTVET RegNo, certificate, region, n.k.), (3) Pakia picha, video, programs, na fee structure, (4) Wasilisha kwa uhakiki, na (5) Ukithibitishwa, chuo chako kitaonekana kwa umma.
2 Nini kinahitajika ili chuo changu kithibitishwe?
Ili chuo chako kithibitishwe kinahitaji: (1) NACTVET RegNo halali, (2) NACTVET Certificate (PDF), (3) Taarifa kamili za chuo (jina, region, ownership, n.k.), (4) Program angalau moja, (5) Logo na cover image, (6) Maelezo ya chuo (about), na (7) Fee structure. Baada ya kukamilisha, SuperAdmin atahakiki na kuthibitisha.
3 Gharama ya lead ni kiasi gani?
Gharama ya lead ni TZS 2,000/= kwa mwanafunzi mmoja. Unalipia tu baada ya kukubali lead na kuona taarifa za kielimu za mwanafunzi. Ukilipia, unapata taarifa kamili za mawasiliano (simu, email, anwani).
4 Je, ninaweza kukataa lead?
Ndiyo, unaweza kukataa lead yoyote. Lakini kumbuka: kila lead unayokataa inaathiri ranking score yako. Vyuo vinavyokataa leads nyingi vinapata ranking ya chini. Hii inasaidia kuhakikisha vyuo vinajibu maombi yote.
5 Nini kinatokea kama chuo hakitajibu maombi kwa siku 30?
Kama chuo hakitajibu maombi (application fee) kwa siku 30, ASACOHUB inatoa warning. Kama bado hakijajibu, chuo kinaweza kubanwa (banned) na profile yake kuondolewa kwenye jukwaa. Hii inalinda wanafunzi na kuhakikisha ubora wa huduma.
6 Ninawezaje kuongeza capacity ya chuo changu?
Unaweza kubadilisha capacity ya chuo chako kwenye dashboard yako ya chuo. Nenda kwenye "Settings" au "Capacity" na uweke idadi mpya ya wanafunzi unaoweza kuchukua. Mabadiliko yanaonekana mara moja kwenye profile yako.

Hukupata Jibu Unalolitafuta?

Wasiliana nasi moja kwa moja na timu yetu itakusaidia haraka.

Uko Tayari Kuomba?

Fungua akaunti yako bure na anza kuomba vyuo hadi 3.