ASACOHUB
ASACOHUB
ASACHIFU COLLEGES HUB, Loading....
📞 +255 679 852 485  |  ✉ info@asacohub.ac.tz
About Contact Help
About ASACOHUB

Tunakuunganisha na Chuo Sahihi, kwa Njia Rahisi na ya Kuaminika.

ASACOHUB ni jukwaa la kidijitali linalounganisha wanafunzi wanaotafuta vyuo na vyuo vinavyotafuta wanafunzi. Tunatoa mfumo rahisi wa kuomba, kufuatilia maombi, na kupata taarifa sahihi za vyuo vyote vilivyosajiliwa na NACTVET.

1+ Verified Colleges
2+ Programs Available
1+ Registered Students

Dhamira, Maono, na Maadili

Misingi inayotuongoza katika kuwahudumia wanafunzi na vyuo Tanzania.

Dhamira Yetu

Kuwezesha kila mwanafunzi Tanzania kupata chuo kinachofaa kwa urahisi, kwa kutoa mfumo rahisi, wa kuaminika, na wa kidijitali wa kuomba na kufuatilia maombi ya vyuo.

Maono Yetu

Kuwa jukwaa namba moja la kuunganisha wanafunzi na vyuo Afrika Mashariki, likitoa fursa sawa kwa kila mwanafunzi, popote alipo.

Maadili Yetu

  • Uadilifu na uwazi
  • Urahisi kwa mtumiaji
  • Usalama wa taarifa
  • Ubora wa huduma
  • Uwiano kwa wote

Jinsi ASACOHUB Inavyofanya Kazi

Hatua rahisi kwa wanafunzi na vyuo kuanza kutumia jukwaa letu.

01

Jisajili

Fungua akaunti bure kwa jina lako, barua pepe, na namba ya simu. Thibitisha kwa OTP.

02

Kamilisha Wasifu

Jaza taarifa zako za elimu, region, na documents. Subiri uthibitisho wa ASACOHUB.

03

Tafuta Chuo

Vinjari vyuo vilivyothibitishwa, chuja kwa Health/Non-Health, region, na ownership.

04

Omba

Omba vyuo hadi vitatu. Chagua program unayotaka na wasilisha maombi yako.

05

Fuatilia

Fuatilia hali ya maombi yako na pokea taarifa kwa SMS na Email.

06

Pata Joining Instructions

Ukiidhinishwa, pakua joining instructions moja kwa moja kwenye akaunti yako.

01

Jisajili Chuo

Fungua akaunti ya chuo kwa jina la mwakilishi na taarifa za chuo.

02

Wasilisha KYC

Pakia NACTVET RegNo, certificate, picha, program, na fee structure.

03

Thibitishwa

ASACOHUB inahakiki na kuthibitisha chuo. Baada ya hapo, chuo kinaonekana kwa umma.

04

Pokea Leads

Pokea maombi ya wanafunzi kama leads, uone taarifa zao za kielimu (bila contacts).

05

Lipia Lead

Kubali lead na ulipie TZS 2,000 kupata taarifa kamili za mawasiliano.

06

Karibisha Mwanafunzi

Wasiliana na mwanafunzi, fanya admission, na pakia joining instructions.

Kwa Nini Uchague ASACOHUB?

Sababu sita zinazotufanya tuwe jukwaa bora la kuunganisha wanafunzi na vyuo.

Vyuo Vilivyothibitishwa

Vyuo vyote kwenye ASACOHUB vinahakikiwa na kuthibitishwa. Hakuna vyuo vya uongo.

Urahisi wa Kuomba

Omba vyuo hadi vitatu kwa mchakato rahisi, bila usumbufu wa karatasi.

Taarifa kwa Wakati

Pokea taarifa za maombi yako kwa SMS na Email, wakati wowote.

Usalama wa Taarifa

Taarifa zako zinalindwa kwa teknolojia ya kisasa. Contacts zinaonekana kwa chuo tu baada ya kulipia lead.

Ranking ya Vyuo

Vyuo vinapangwa kwa utendaji, siyo idadi ya leads pekee. Hii inakuza ubora.

Msaada wa Muda Wote

Timu yetu ipo kukusaidia wakati wote, kwa simu, barua pepe, au WhatsApp.

1+ Colleges
2+ Programs
1+ Students
1+ Applications

Aina za Vyuo

ASACOHUB ina vyuo vya aina mbili kuu, vyote vilivyothibitishwa na NACTVET.

Wasiliana Nasi

Una swali, malalamiko, au unahitaji msaada? Tuko hapa kukusaidia.

Simu

Piga au tuma SMS wakati wowote.

+255 679 852 485

Barua Pepe

Tuma barua pepe na utapata jibu haraka.

info@asacohub.ac.tz

WhatsApp

Wasiliana nasi kwa WhatsApp kwa msaada wa haraka.

Chat Nasi

Ofisi

Karibu ofisini kwetu kwa mazungumzo ya ana kwa ana.

Arusha, Tanzania

Uko tayari kuanza?

Jiunge na maelfu ya wanafunzi wanaotumia ASACOHUB kupata vyuo bora.

Uko Tayari Kuomba?

Fungua akaunti yako bure na anza kuomba vyuo hadi 3.