ASACOHUB
ASACOHUB
ASACHIFU COLLEGES HUB, Loading....
📞 +255 679 852 485  |  ✉ info@asacohub.ac.tz
About Contact Help
FAQ

Maswali Yanayoulizwa Sana

Hapa utapata majibu ya haraka kwa maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu ASACOHUB, wanafunzi, vyuo, malipo, na usalama.

27 Maswali 5 Makundi

Maswali ya Jumla

Maswali 5 kwenye kundi hili

1 ASACOHUB ni nini?
ASACOHUB ni jukwaa la kidijitali linalounganisha wanafunzi wanaotafuta vyuo na vyuo vinavyotafuta wanafunzi Tanzania. Tunatoa mfumo rahisi wa kuomba vyuo, kufuatilia maombi, na kupata taarifa sahihi za vyuo vyote vilivyosajiliwa na NACTVET.
2 ASACOHUB inasaidia nani?
ASACOHUB inasaidia watu wawili wakuu: (1) Wanafunzi wanaotafuta vyuo vya kujiunga, na (2) Vyuo vinavyotafuta wanafunzi. Pia inasaidia wazazi na walezi wanaotafuta taarifa za vyuo kwa ajili ya watoto wao.
3 ASACOHUB ipo wapi?
ASACOHUB ina ofisi zake Arusha, Tanzania. Lakini huduma zetu zinafanyika mtandaoni (online) kote Tanzania. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu, barua pepe, au WhatsApp wakati wowote.
4 Je, ASACOHUB inashirikiana na NACTVET?
ASACOHUB inaonyesha vyuo vilivyosajiliwa na kuthibitishwa na NACTVET. Tunahakikisha kila chuo kwenye jukwaa letu kina NACTVET RegNo halali na certificate. Hii inasaidia wanafunzi kuepuka vyuo vya uongo.
5 Ninawezaje kuwasiliana na ASACOHUB?
Unaweza kuwasiliana nasi kwa njia nne: (1) Kupiga simu +255 679 852 485, (2) Kutuma barua pepe info@asacohub.ac.tz, (3) WhatsApp kwa namba hiyo hiyo, au (4) Kutembelea ofisi zetu Arusha. Unaweza pia kutumia fomu ya Contact Us kwenye tovuti yetu.

Hukupata Jibu Unalolitafuta?

Wasiliana nasi moja kwa moja na timu yetu itakusaidia haraka.

Uko Tayari Kuomba?

Fungua akaunti yako bure na anza kuomba vyuo hadi 3.