ASACOHUB
ASACOHUB
ASACHIFU COLLEGES HUB, Loading....
📞 +255 679 852 485  |  ✉ info@asacohub.ac.tz
About Contact Help
FAQ

Maswali Yanayoulizwa Sana

Hapa utapata majibu ya haraka kwa maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu ASACOHUB, wanafunzi, vyuo, malipo, na usalama.

27 Maswali 5 Makundi

Usalama na Faragha

Maswali 5 kwenye kundi hili

1 Taarifa zangu zinalindwa vipi?
Taarifa zako zinalindwa kwa: (1) Kusimbwa kwa password (bcrypt), (2) CSRF protection kwenye forms zote, (3) SQL Injection prevention kwa PDO, (4) XSS protection, (5) OTP kwa uthibitisho wa simu, na (6) Encryption ya taarifa nyeti. Hatuweki taarifa zako kwa watu wa tatu bila idhini yako.
2 Nani anaweza kuona taarifa zangu?
Taarifa zako zinaonekana kwa: (1) Wewe mwenyewe, (2) ASACOHUB SuperAdmin kwa uhakiki, na (3) Vyuo ulivyo omba — lakini contacts zinaonekana tu baada ya chuo kulipia lead. Hatuweki taarifa zako kwa vyuo visivyolipia lead.
3 Kwa nini mnataka NIDA number yangu?
NIDA number ni hiari (optional). Tunaiomba ili kuhakikisha utambulisho wako na kupunguza udanganyifu. Kama hutaki kuitoa, unaweza kuacha wazi. Hata hivyo, kuitoa inasaidia kuhakikisha usalama wa akaunti yako.
4 Je, mnashiriki taarifa zangu na serikali?
Hatushiriki taarifa zako na serikali isipokuwa kama sheria inatulazimu kufanya hivyo (kwa mfano, amri ya mahakama). Tunazingatia sheria za Tanzania kuhusu faragha ya taarifa (Data Protection).
5 Ninawezaje kubadilisha password yangu?
Unaweza kubadilisha password yako kwenye profile yako. Nenda kwenye "Settings" au "Account" na uchague "Change Password". Utahitajika kuweka password ya sasa, kisha password mpya. Password mpya lazima iwe na angalau herufi 8.

Hukupata Jibu Unalolitafuta?

Wasiliana nasi moja kwa moja na timu yetu itakusaidia haraka.

Uko Tayari Kuomba?

Fungua akaunti yako bure na anza kuomba vyuo hadi 3.